Wajibu wa elimu kwa raia, wakati ambapo inaweza kutokana na sheria au taarifa waza kuhusu malengo, inaweza kutokea kwa au kushawishiwa na tamaduni za kimataifa zinazohusiana nayo na vifaa na kanuni zilizowekwa na nchi katika mabaraza na mkataba ya kimataifa.
Mjadala kamili kuhusu kanuni hizi na mahusiano yake na uchaguzi zinapatikana katika chapisho la Kituo cha Umoja Wa Kimataifa kuhusu Haki za Kibinadamu.
[1] Katika uchunguzi wake katika vyombo kumi na tisa vya kilimwengu na vya kimajimbo, chapisho linaeleza kuwa “nchi na watu ulimwenguni kote wametambua kuwa chaguzi huru na za haki ni hoja muhimu katika shughuli ya uteteji wa demokrasia na njia ya haraka ya kuelezea nia ya watu.
[2]
Ili kuweza kuafikia haya, chapisho linavuta makini kwa kile ambacho inaonelea kuwa sifa za kawaida za sheria ya uchaguzi na taratibu ambazo huhakikisha kuwa chaguzi zinafanyika kwa njia huru na ya haki na chini ya kanuni za kisheria. Kuhusu habari kwa umma na elimu kwa Wapigakura, nyaraka inaeleza:
124. Ufadhili na utawala / usimamizi unafaa kutolewa kwa kampeni za elimu na habari kwa Wapigakura ambayo ni huru na isiyopendelea. Elimu kama hiyo ni muhimu sana hasa kwa jamii zenye tajiriba ndogo au zisizo na tajriba yoyote ya chaguzi za kidemokrasia. Umma unafaa kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu wapi, lini na jinsi ya kupiga kura, na vilevile umuhimu wa kupiga kura. Wanafaa kuwa na imani katika uadilifu wa mchakato na haki yao ya kushiriki katika mchakato huo.
125. Maandishi yanafaa kuwepo kwa wingi na yanafaa kuchapishwa katika lugha mbalimbali za kitaifa ili kusaidia kuhakikisha ushiriki wa maana wa Wapigakura wote waliohitimu. Mbinu nyingi za vyombo vya habari zinafaa kuhusishwa ili kutoa elimu ya uraia mwafaka kwa watu wenye viwango tofauti vya elimu. Kampeni kuhusu elimu kwa Wapigakura zinafaa kuenea katika eneo zima la nchi, yakiwemo maeneo ya mashambani na ya mbali.
[3]
Baraza kuu la Jumuiya ya Madola pia limehusika katika Mipango kadha ya kusaidia uchaguzi katika Jumuiya ya Madola yote. Kati ya mwaka wa 1993 na 1997 iliandaa mikutano mbalimbali ya Maafisa Wakuu wa Uchaguzi wa jumuiya ya Madola ambapo walifanya majadiliano kuhusu tamaduni au taratibu bora. Kwa kuzingatia mijadala hii na vifaa (vya kimaandishi) vilivyonakiliwa, walitengeneza nyaraka kuhusu taratibu za uchaguzi yenye mada Maadili Bora ya Uchaguzi katika Jumuia ya Madola [4]. Mbali na umuhimu wa nyaraka hii, mijadala yenyewe ilikuwa msingi muhimu wa kubadilishana habari na tajriba.
Kanuni zilizoelezwa katika nyaraka yenyewe zinatumika sio tu kwa uchaguzi wa mashinani na kitaifa, bali pia zinadhamiriwa kusaidia watu katika kuipa nguvu mifumo yao ya uchaguzi. Kwa hivyo, kanuni hizi zinawasilishwa kama vifaa na sio maagizo ya mwisho. Zingatia aya mbazo zinahusiana na elimu kwa umma.
42. Mifumo ya elimu kwa umma iliyo mwafaka na isiyokuwa na miegemeo, japo kila mara si wajibu wa tume ya uchaguzi, ni sifa muhimu katika nchi ambapo “utamaduni” wa kupiga kura bado unakuzwa na vilevile katika demokrasia zilizoimarika. Kwa hivyo, Mipango hiyo inafaa kufadhiliwa kikamilifu na kupewa mpangilio wa kitaalamu. Pia Mipango hiyo inafaa kulenga makundi mahususi (kama vile wanawake, jamii ndogo, wenye upungufu, na watoto wa shule). Pale inapowezekana, tamaduni za uchaguzi wa kitaifa zinaweza kukuzwa katika taratibu za uchaguzi shuleni na vituo vya elimu ya uchaguzi vinaweza kuanzishwa katika maeneo yafaayo.
43. Uhimizaji, hasa, wa ushiriki wa wanawake katika shughuli zote za mchakato wa kidemokrasia unastahili uzingatifu maalum.
44. Gharama ya Mipango ya elimu kwa umma inafaa kupunguzwa kupitia kwa kutoa vifaa vya utangazaji wa huduma za umma kwa malipo ya chini au bila malipo yoyote.[5]
Nyaraka ya Jumuiya ya Madola inaenda zaidi ya taarifa ya Umoja wa Mataifa katika kutambua umuhimu wa elimu kwa Wapigakura katika “demokrasia zilizoimarika”. Kati ya 1994 na 1997 ongezeko la hali ya kuvutiwa kwa watu kuhusu utendakazi wa demokrasia na ushiriki – na hasa kujitokeza kwa Wapigakura na shauku – baina ya demokrasia zinazochipuza na zilizoimarika ilidhihirisha kuwa demokrasia haiwezi kupuuzwa katika hali yoyote ile.
Kutokana na hayo, kuna makubaliano ya kijumla na ya kimataifa kuhusu umuhimu wa elimu kwa Wapigakura na haja ya kuanzisha Mipango yenye gharama nafuu na ya kitaalamu katika kuunga mkono chaguzi. Hili pia linachangia katika kuunga mkono ajenda pana ya uendelezaji wa demokrasia.
Makundi ya wachunguzi ya kimataifa kama yanavyotarajiwa hutoa maoni yao kuhusu ukamilifu wa Mipango ya elimu kwa Wapigakura na uandaaji wa Wapigakura. Taarifa hizi huzidisha uelewa wetu wa kile kinachohitajika ili kuhakikisha sio tu uchaguzi huru na wa haki lakini pia msingi unaofaa kwa kufanya maamuzi ya kidemokrasia na uongozi katika mazingira changamano.
Maelezo:
[1] Kituo cha Haki za Kibinadamu, Haki za Kibinadamu na Chaguzi – Kijitabu maalumu Masuala ya Kisheria, Kiufundi na Haki za Kibinadamu katika, Mfululizo wa Mafunzo ya Kitaalamu; Nambari 2 (New York na Geneva: Umoja wa Mataifa, 1994), 1.
[2] Kama hapo juu.
[3] Kama hapo juu., 17.
[4] Baraza kuu la Jumuiya ya Madola, Maadili Bora ya Uchaguzi katika Jumuia ya Madola, Nyaraka za Utendakazi, (London: Baraza kuu la Jumuiya ya Madola, 1997),
[5] Ibid., aya; 42 – 44.