Vyama vya kisiasa vinasalia kuwa na kiungo muhimu sana cha mfumo wa siasa za kidemokrasia katika serikali ya karne ya 21.
Kumekuwa na mwelekeo wa kiajabu wa kupuuza mchango ambao wa vyama vya kisiasa vinaweza kufanyia elimu kwa wapigakura na ambao vinapaswa kutoa kwa shughuli nzima ya elimu kwa raia. Hali ya kutojali kwa mpigakura ina uhusiano wa moja kwa moja na ufaafu wa vyama vya kisiasa katika kujenga na kuwasilisha misimamo ya kisera ambayo huimarisha ari ya raia kushiriki katika maswala ya umma na serikali na ambayo kwa sababu ya utendakazi wake katika kushughulikia mahitaji ya watu binafsi na jamii zao huweka teuzi mikononi pa watu ambazo huwachochea kujitokeza na kupiga kura.
Mwelekeo huu umechochewa na imani kwamba wale walio na nia fulani hawapaswi kuaminiwa kuwaarifu wapigakura kuhusu haki zao au kuwasaidia katika kufanya maamuzi, na kwa kawaida huenda zikajaribu kuwarai na kuwalaghai kwa kutoa taarifa za upande mmoja au hata habari zisizo na ukweli. Hali kwamba mtu anaweza kuyaamini mashirika kama hayo kuongoza bali si kuwa nia kuteka fikra za umma wakati mwingine.
Hata hivyo, hata kama watu binafsi yanaenenda katika njia hii, usambaaji wa wazi wa habari na viwango ambamo chaguzi za kisasa zinaweza na zinapaswa kufanywa hutoa nafasi kwa jumbe na taarifa shindani kuwafikia wapigakura. Hivyo basi kuna mifumo mingine ambamo huchukuliwa kwamba juhudi za ushirikiano katika makundi yanayofanya kampeni na shirika mwafaka lililogatuliwa la kusimamia uchaguzi yanaweza kutoa habari za kutosha kuhusu uchaguzi na elimu kwa raia katika uchaguzi wowote ule.
Hivyo basi kusababisha uchache unaodhihirika wa elimu kwa wapigakura katika demokrasia zilizokita mizizi na msisitizo unaotolewa kuhusu elimu kwa wapigakura katika nyakati za mabadiliko pekee. Huu bilashaka ni mwelekeo usio na maono unaoendelea kuongezeka na kupuuza asasi nyingine nyingi katika demokrasia zilizokita mizizi kama hizo ambazo hutekeleza mipango ya elimu nyakati za uchaguzi bila kuwaelekeza kwa hughuli ya elimu kwa wapigakura.
Waelimishaji wanaowajibikia mipango ya elimu kwa wapigakura au raia wanapaswa hivyo basi kuzingatia kwa uangalifu mbinbu bora ya kuhusisha vyama vya kisiasa katika kuchangia kwenye mpiango yao, iwe ni kwa njia ya moja kwa moja ya mtaala mmoja, kwa kuhimiza wafuasi wavyo kushiriki katika mipango hiyo, kwa kubuni na kutekeleza mipango yao binafsi ya elimu jinsi inavyofanywa na mshirika mengi au pengine kwa kuchukulia haja ya kuwasiliana vilivyo na kwa juhudi na umma katikati ya na wakati wa uchaguzi kuhusu mipango yao wenyewe na kuhusu mazingira ya kikatiba yanayowaunganisha na mifumo na mienendo fulani ya mashirika na kisha kuwapa uhuru wa kuwepo na kushindana.
Katika nchi ambamo vyama vuya kisiasa ni maskini sana, waelimishaji wanaweza hata kuangazia njia nyingine zisizoegemea upande wowote ambazo zinaweza kutumiwa kuimarisha kampeni. Miongoni mwa vibadala vya njia hizi ni:
- Kuwafundisha wagombea pamoja na vyama vyao katika kumudu na kutekeleza kampeni
- Vituo huru vya kuchapisha na kusambaza manifesto za vyama
- Kupigia kampeni uwezo kufikia chombo cha habari kinachoendeshwa na serikali
- Kuvipa vyama vijitabu vya taarifa zisizobagua kuhusu wapigakura ambavyo wanaweza kutumia kuongeza taarifa yao ya kibinafsina kupunguza gharama za uchapishaji.
- Kufanya shughuli za kuelimisha umma ambamo wagombea na vyama vinaweza kujitambulisha kwa umma.
Tathmini ya wajibu unaoweza kutekelezwa na waelimishaji wa vyama vya kisiasa itataka kuzingatia kiwango ambapo vyama vinavyowakilishwa wakati huo katika mabunge mbalimbalivinawakilisha raia kwa jumla na kama kupitia kwa kasoro kwenye mfumo wa uchaguzi au kutokana na tofauti na kutengwa kijamii na kiuchumi, kuna vyama vilivyoundwa rasmi, viwe vimesajiliwa au la,au makundi na miungano isiyo rasmi ya kisiasa, ambayo pia inapaswa kujumuishwa katika shughuli hiyo kielimu. Maingiliano na makundi kama hayo yatategemea nafasi ya mwelimishaji huyo katika asasi hiyo. Ikiwa sehemu fulani ya shirika la kisheria huenda wakakosa kuruhusiwa kutangamana na chama chote kilichosajiliwa: japo kama hii ndiyo hali, wanapaswa kuzingatia njia nyingine za kuhakikisha kwa mipango ya kielimu haiwatengi watu ambao kwa sababu ya ufuasi wao kwa vyama vya kisiasa wanaweza kukosa kufikiwa kama ni kwa mipango mingine ya maafisa wa kuelimisha wasioegemea upande wowote.