Watu mbalimbali wana mahitaji tofauti tofauti ya kielimu. Wakati ambapo mahitaji mengine yanaweza kuwa ya kijumla kwa Wapigakura wote, kuna uwezekano kwamba hata haya mahitaji yanaweza kuwasilishwa kwa njia tofauti na makundi mbalimbali.
Ni nani atakayefaidika kwa mipango ya kielimu?
Tathmini ya mahitaji lazima izingatie wapokezi au wafaidi wa Mipango ya kielimu. Kuna maneno kadhaa ambayo yanaweza kutumiwa kuwarejelea hawa wapokezi. Kila neno lina uzuri na ubaya wake, na waelimishaji wanaofanya kazi pamoja wanaweza kukanganywa na istilahi hizi.
Wataalamu wa mawasiliano wanazungumza kuhusu “umma” au “raia”, kwa maana ya kikundi cha watu walio na sifa fanani. Watangazaji wa kibiashara watazungumzia “hadhira” kama vile “hadhira ya vijana”. Wenye kutekeleza kampeni au walio na ujumbe mahsusi kwa umma wanaweza kuzungumzia “makundi lengwa” au “hadhira lengwa” kama vile wanawake wa mashambani. Na watetezi wengine au wakufunzi wanaweza kuzungumzia “maeneo” wanaofanya kazi nao.
Kila neno linatumika kutia umuhimu wa kufafanua kwa makini na kugawanya kwa hakika iwezekanavyo kila kundi mahsusi ambalo mkufunzi anapania kufanya kazi nao. Hata ingawa jukumu la elimu kwa mpiga kura ni bia, na waelimishaji wana wajibu wa kuarifu Wapigakura kwa (tazama Makundi yenye Athari Kuu), Mipango lazima izingatie njia na ujumbe mbalimbali kwa makundi tofauti tofauti ya watu. Huenda makundi mengine yamebaguliwa na mengine kuwa na mahitaji spesheli kwa mujibu wa michakato ya upigaji kura. (tazama Wapigaji kuraWaliobaguliwa na Makundi yenye Mahitaji Spesheli). Zaidi ya mahitaji ya habari ya kila kikundi, lengwa, itatokea hali ambapo baadhi ya makundi yatasoma tofauti na wengine.
Matatizo ya ugawaji katika makundi
Kuna matatizo kwa chaguo walionalo waelimishaji. Baadhi ya matatizo haya yanahusiana na habari na rasilimali. Haiwi rahisi kila wakati kujua na kukisia kuhusu watu au makundi ya watu na kuweka watu pamoja kwamba huishia kurahisisha mambo.
Matatizo mengine yanaletwa na mazingatio ya kisiasa, kikatiba na utengenezaji wa sheria. Mwelimishaji wa uchaguzi anaweza kuwajibika kisiasa au kisheria kushughulikia hadhira au maeneo mahususi. Hata ingawa kunaweza kuwa na mazingatio mengine ya kifedha na harakati. Rasilimali zinazohitajika kufikia kikundi kidogo cha wafugaji au wahamiaji, kwa mfano zinaweza kukosekana, hata ingawa kikundi hicho kinaweza kuwa kimejizingatia au kimezingatiwa na wengine. Au Mipango ya elimu kwa Wapigakura inaweza kuwa jumlishi- kupitia lugha iliyochaguliwa, njia au methodolojia- ambayo inaweza kuwa imebagua kundi fulani katika jamii.
Waelimishaji wa elimu kwa Wapigakura sharti wawe na “sifa” fulani ambazo zimefanywa bayana kwa kutathmini maeneo yatakayo lengwa na kwa kiasi gani. Waelimishaji wanaweza kuhisi kwamba vitu hivi vyote vina usawa, watu maskini wanahitaji uangalifu zaidi kuliko watu matajiri hata ingawa wote wanahitaji elimu. Au wanaweza kuamini kwamba ushirika wa wanawake katika upigaji kura ni muhimu kuliko ule wa wanaume. Katika nyingi za chaguo hizi, huenda kuna uwezekano wa kuanzisha Mipango ya kielimu isiyobagua lakini ambayo imejengeka kwenye ubora wa wakufunzi mahsusi wa kufanya kazi katika maeneo fulani. Hivi vilevile ni “vikundi vya athari kuu” ambavyo waelimishaji watakaofikia kwa sababu matokeo yanayoweza kuafikiwa kwa kushughulikia makundi kama hayo. Waelimishaji walio na makini kwa kupanua na kuendeleza demokrasia, wanawake pia kuchagua kuelekeza juhudi zao kwa makundi “yaliyobaguliwa” kama yale yaliyozungumziwa hapo juu (ambayo gharama zao mara nyingi huwa juu) na ambayo huhitaji Mipango maalum.
Mpigaji kura binafsi
Istilahi hizi- lengwa, hadhira, zote ni istilahi jumulishi. Istilahi hizi zinaweka watu katika makundi yenye kategoria mbalimbali. Hata hivyo waelimishaji hupendelea kutoweka watu katika makundi na badala yake wao huwazingatia kama waelimishaji, washiriki au wasomi. Waelimishaji katika elimu ya uchaguzi huandaa Mipango na mwongozo wa mafunzo. Na hao watakao wazia jukumu lao kama kampeni, habari ya umma na vipindi. Kuna nyakati ambapo watalazimika kutumia istilahi jumlishi. Lakini wakufunzi bora watakuwa wakiwaita tena kila mwanafunzi binafsi kwenye msingi wa Mipango.