Waelimishaji hasa wanaofanya kazi katika Mipango rasmi ya elimu ya Wapigakura, ama kupitia mamlaka ya uchaguzi au mashirika mengine ya kiserikali, watakuwa na majukumu ya kutoa habari kwa Wapigakura wa kijumla. Wanaofaa kupiga kura watafafanuliwa katika katiba na kwenye sheria ya uchaguzi. Kwa hakika uraia, umri na mahitaji ya uwezo vinaundwa.Wafungwa wengine wanaweza kurejesha hali zao ilhali wengine hawatafanya hivyo. Katika baadhi ya uchaguzi wa manispa au uchaguzi wa wawakilishi kulingana na wilaya, mahitaji ya makazi pia yatazingatiwa.
Mamlaka ya uchaguzi yanaweza kuwa na majukumu mengineyo, kisha yale ya kujuza Wapigakura kuhusu tarehe, aina ya uchaguzi, masaa ya uchaguzi, vituo vya kupigia kura, mahitaji ya kujisajili na maeneo, aina ya vitambulisho vinavyohitajika kupimia uwezekano wa mtu kupiga kura, njia mwafaka ya kubainisha uchaguzi wa mtu kwenye karatasi ya kupigia kura, na mengine mengi.
Habari hii ya jumla kuhusu ya uchaguzi inaweza kuongezewa, ama na mamlaka ya uchaguzi kupitia mipango yake au wanachama wa mashirika ya kielimu kwa hali za kipekee kwa makundi yaliyobaguliwa au yenye mahitaji spesheli.