Waelimishaji wenyewe wanaweza kupunguza juhudi zinazohitajika kuendeshea Mipango kwa kutambua makundi ya watu ambao wenyewe wanaweza kuwa na athari kuu kwa wengi bila kuwekeza juhudi nyingi kwao katika mipango ya elimu. Kuna mwongozo wa Mipango unaosema kwamba shughuli za masomo zipimwe katika viwango viwili-juhudi na athari. Wakufunzi katika elimu ya uchunguzi wakitumia viwango hivi, watakuja kugundua kwamba kazi yao itagawika katika aina nne:
- Mipango inayotumia juhudi nyingi na ina athari kuu.
- Mipango inayotumia juhudi nyingi na ina athari kidogo.
- Mipango inayotumia juhudi kidogo na ina athari kuu.
- Mipango inayotumia juhudi kidogo na ina athari kidogo.
“Juhudi” inaweza kufafanuliwa kama matumizi ya rasilimali (watu, fedha,vifaa) na uchangamani wa Mipango. “Athari” inaweza kufafanuliwa kama kufikia malengo ambapo matokeo yake ni mabadiliko katika mienendo, tabia, ujuzi au habari kwa hadhira lengwa. Hivyo waelimishaji wenye hekima watahitaji kuendesha Mipango inayopunguza juhudi huku hadhari ikiongezeka.
Sharti pawe na unyenyekevu katika kuchagua makundi yenye athari kuu. Uchaguzi wa makundi haya ni sanaa na wala siyo sayansi. Kuna uwezekano kwa waelimishaji kujishawishi kwamba wamechagua makundi kama hayo wakati ambapo kundi lengwa limechaguliwa kimsingi kwa ajili ya upunguzaji wa juhudi badala ya wakufunzi kujuwa kwamba kutakuwa na ongezeko la athari.
Waelimishaji Wanatafuta Nini?
Kama kanuni ya kijumla, wakufunzi watakuwa wanatafuta watu (au makundi ya watu), ambao tayari wamepata wengine na wanafurahia uaminifu na heshima katika maeneo. Wazungumzapo watu hutilia maanani wanayoyasema. Muhimu pia, wana makundi ya watu ambao wanataka kuwasikiliza. Wakufunzi wanaweza kutafuta watu wenye mamlaka kupitishia ujumbe kwa maeneo mahsusi. Kitaalamu wanaweza kuwa walimu, wakufunzi au wataalamu wa mawasiliano. Au wanaweza kuhamasisha watu kupitia nyadhifa zao kwenye kampuni na asasi.
Ubora wa kutumia wakati wa kutambua makundi kama hayo ya watu kisha kuwapa mazingatia ni muhimu. Lakini cha kushangaza, waelimishaji huendelea kuandaa Mipango ya kijumla kutunzia “ugawanyaji” kama mtindo licha ya kwamba mtindo huo huweza kuwa ghali, hata hivyo ilivyo sasa mtindo huo kwa mtu mmoja huwa nafuu kigharama.