Katika kila uchaguzi na kwa yakini kila Mipango kwa Wapigakura, makundi maalum wanao hitaji mazingatio mahsusi. Kuna makundi mengine ambayo yamekuja kuwa kasi sana.Makundi haya ni kama vili;
- Wafanyikazi katika shughuli ya uchaguzi.
- Wapigakura walio ughaibuni.
- Wapigakura wasiokuwepo.
- Wahamiaji na wakimbizi wa ndani kwa ndani.
- Wafugaji na wakimbizi.
- Wapigakura walio sehemu mbali
- Walio wachache katika jamii.
- Watu walemavu
- Wapigakura walio kwenye manyumbani na hospitali.
- Wafungwa sugu.
- Wafungwa wa kisiasa
- Walinda usalama
- Wanawake
- Vijana na Wapigakura kwa mara ya kwanza.
Orodha hii haimaanishi kwamba hakuna makundi mengine ambayo yanaweza kuhitaji mazingatio maalum. Makundi haya yatatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Jamii inapo kuwa na migao midogo midogo kupitia maendeleo, na kutambua zaidi mahitaji maalum na haki za kibinadamu ya makundi kuliko zile za watu binafsi, ni wazi kwamba makundi mengine zaidi Katika hali ya kimabadiliko, mivuto ya baadhi ya makundi yatatambuliwa kwa ukaribu na makundi haya yatahitaji mazingatio maalum wakati wa uchaguzi. Kanuni ya Khmer Rouge kule Kambodia, kwa mfano ilileta idadi kubwa ya wakimbizi wa Kambodia ambao walisaidiwa kwa uchaguzi uliosimamiwa na umoja wa mataifa. Katika hali ya Bosnia, kulikuwa na makubaliano ya Dayton ambayo yalihitaji kwamba wakimbizi wa ndani kwa ndani ambao wamesaidiwa kupata makazi ambayo yamepangwa na shirika la usalama na mashirikiano ya ulaya. Uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa Afrika Kusini ulinuiwa kuwa jumlishi na hivyo ilibidi mipango kuwekwa kwa wananchi wa Afrika Kusini walioko ughaibuni kushiriki. Katika demokrasia ambazo zimedumu wakati Wapigakura hasa vijana wanaposusia kushiriki upigaji kura. Kuna sababu tosha za kutoa elimu kwa Wapigakura pamoja na kuweka mipango ya kuhamasisha vijana.
Waelimishaji hawawezi kupuuza njia za wazi za kijadi za jamii na ambazo kwazo jamii hutenda kazi iwapo wanatazamia kuendeleza demokrasia kwa wananchi wote. Licha ya uhusiano wa karibu ulioanzishwa na makundi mahsusi ya wananchi kupitia lugha, utamaduni na mabadiliko ya kimamlaka, elimu tosha huhitaji kwamba maneno tofauti tofauti maalum na mitazamo tata ya watu binafsi.
Wafanyikazi wa Shughuli ya Uchaguzi
Wafanyikazi wa shughuli ya uchaguzi na makamishna wa kusimamia uchaguzi wanaweza kuwa wenye manufaa kuu katika mipango ya elimu. Kundi hili lina ubora wa kuweza kutambuliwa vizuri, lina utashi wa kuhudhuria mafunzo na matukio mengine, wapo hasa kabla ya na iwapo rekodi zinawekwa kutangulia uchaguzi, wana motisha hata ingawa wakati mwingine motisha hiyo huwa ni ya muda kwa kuwapa wafanyakazi wa uchaguzi na maafisa wa uchaguzi pamoja na makamishna wa uchaguzi mafundisho yanayojumlisha komponenti inayo shughulika na elimu ya uchaguzi, wafanyikazi hao wanaweza kuwa wenye kutoa elimu isiyo rasmi (Tazama Jukumu la Maafisa wa Uchaguzi). Wakati huo huo, wafanyikazi wa uchaguzi na maafisa wa uchaguzi katika mataifa mengi yanayoendelea pamoja na jamii zilizo katika harakati za mabadiliko huweza kuzidiwa na kazi kwa malipo duni. Kwa hivyo, waelimishaji huenda wakalazimika kuzuia matajio yasiyoweza kuafikiwa.
Kwa sababu ya majukumu ambayo wafanyikazi wa uchaguzi na maafisa wa uchaguzi hutekeleza,hata hivyo, ni muhimu kuzingatia habari spesheli kuhusu wakati na jinsi wanavyoweza kupiga kura ambayo huenda ikawa tofauti na ile inayowekwa kwa Wapigakura wa kijumla.
Hata ingawa ni majukumu madogo, hayapaswi kupuuzwa kwa sababu yanaathiri matumaini yao ya kuzungumzia uchaguzi. Pia, itapunguza wasiwasi kwao hasa shinikizo inapozidi.
Wapigakura Walioko Ughaibuni
Idadi ya Wapigakura watakaokuwa nje ya nchi wakati wa uchaguzi itatofautiana kutoka nchi moja na nyingine. Pia kutakuwepo na sheria zitakazoongoza Wapigakura walio ughaibuni hasa kuhusu uwezo wa kupiga kura, watapigia wapi na katika hali gani.Kundi hili linaweza kujumlisha walioko ughaibuni kwa sababu za kidiplomasia, likizo au kwa ajili ya kibiashara. Kundi hili linaweza kujumlisha wale walio ughaibuni kwa muda wakiwa bado ni wananchi wa nchi zao kulipo wa makazi yao ya kudumu. Inaweza pia kujumlisha wale walio ughaibuni na hawajawahi hata kuishi katika nchi zao licha ya kuwa na uraia wa nchi zao kwa sababu ya kihistoria. Katika nyingi za hali hizi, walio na nia ya kupiga kura wanahitaji kuwasilisha nia hiyo kwa mamlaka ya uchaguzi ya kitaifa au asasi nyingine ya kiserikali. Mipango inaweza kuwekwa ili kuwafikishia habari au vifaa vya kielimu kwao. Habari hii itakuwa tofauti na ile wanayopatiwa Wapigakura wenyeji, kwa kuwa maeneo ya kupigia kura, saa na jinsi ya kupiga huenda zikawa muhimu. Kupiga kura mapema au kupitia barua huenda ikawa njia mojawapo.
Wapigakura Wasiokuwepo na Kupiga Kura Mapema
Kwa watu ambao watakuwepo nchini uchaguzi ukikaribia, lakini wasiwepo siku yenyewe ya uchaguzi njia nyinginezo huweza kutumiwa. Hili huathiri watu ambao ama wamo njiani au wamo ughaibuni kwa shughuli za biashara au likizo. Kwa baadhi ya uchaguzi kama ule wa raia, unaweza kujumlisha watu ambao hawatakuwepo katika maeneo ambayo walisajiliwa kupiga kura siku ya uchaguzi.
Njia mbili za kushughulikia makundi kama hayo ni Wapigakura wasiokuwepo na upigaji kura wa mapema. Upigaji kura wa mtu asiyekuwepo hutokea pale ambapo jambo hili limewasilishwa kwa wakuu wa uchaguzi. Karatsi za kupigia kura huwasilishwa kwa mpiga kura kupitia njia ya sanduku la posta, kisha mpiga kura hutia alama na kisha kurudisha karatasi hiyo kwa wakuu wa uchaguzi. Katika upigaji kura wamapema, Wapigakura huweza kuenda akatika vituo vya upigaji kura mapema au katika ofisi ya kuu ya maafisa wa uchaguzi kupiga kura. Nchi chache pia zimeruhusu Wapigakura ambao hawatakuwepo katika maeneo yao siku ya uchaguzi katika kura ya rais kupata cheti kitakachowaruhusu kupiga kura katika maeneo mengine. Hivyo njia hizi maalum za huduma ya uchaguzi zina mikakati yao ya kipekee na mahitaji yatakapohitajika kwamba Wapigakura wajulishwe.
Wakimbizi na wakimbizi wa ndani kwa ndani
Kwa kiwango kikubwa, makundi ambayo ni vigumu kushughulikia ni Wapigakura walio nje ya nchi au walio nje ya maeneo yao ya kupiga kura kama wakimbizi na wakimbizi wa ndani kwa ndani. Wakimbizi na wakimbizi wa ndani kwa ndani huhamishwa kutokana na sababu za kivita, mizozo baina ya watu na matatizo ya kimazingira. Mambo haya husababisha kupotea kwa vitambulisho na nyaraka za usajili wa Wapigakura, na rekodi, na kutoweza kupiga kura katika maeneo yao ya usajili, pamoja na kushindwa kupata mahala badala wa kupigia kura. Katika uchaguzi wa wabunge na madiwani, utumizi wa ujumlishaji badala ya upigaji kura wa kila mtu huweza kuzua matatizo ya uwakilishaji. Katika nchi za Yugoslavia ya kale pamoja na Caucuse ni baadhi ya mifano michache ya upigaji kura wa kimaalum pamoja na mahitaji ambapo mipango lengwa ya elimu kwa Wapigakura ilihitajika kwa wakimbizi wa nchi jirani na wale wakimbizi wa ndani kwa ndani.
Wakati ambapo ukimbizi umeruka mipaka ya nchi, matatizo huongeza. Wakati uchaguzi ni matokeo ya kusulihisha matatizo ya kisiasa, huenda kukawa na mipango ya kuwarudisha wakimbizi uchaguzi ukikaribia, kama ilivyokuwa Mozambique. Iwapo wakimbizi wanaweza kurudishwa mapema, kabla ya tarehe ya uchaguzi, huenda kukawa na mipango ya elimu ya uchaguzi. Hivyo huweza kutukia kwa wale ambao wamekuwa wakimbizi kwa muda au kwa ajili ya upujufu fulani au vita, hawa huhitaji mazingatio fulani. Habari ya mipango kama hiyo huweza kupatikana katika sehemu ya Mawasiliano na Wahamiaji, Wakimbizi wa nje na Wakimbizi wa ndani kwa ndani.
Wafugaji na wahamiaji
Uchaguzi wa kitaifa, kimaeneo na wa manispa huchukuliwa kama ule wa kuwachagua wawakilishiwa maeneo fulani ya kijiografia. Hata hivyo kuna wale ambao husafiri na ambao hawawezi kufungwa katika eneo fulani kwa kuwa na mivuto ya maeneo mengi, na pia wasioweza kubanwa kwa wilaya au eneo moja. Wahamiaji na wafugaji hawa japo wamelazimishwa na mtindo wao wa kimaisha, wanaleta changamoto (kupitia mitazamo isiyo pingamizi) kwa dhana za kidemokrasia.
Pia wanatia changamoto kwa waelimishaji. Kwa kiwango kikubwa jamii wanaounda na ambayo kwayo wao huunda ruwaza za uongozo wao huwa imefungwa kwa wageni. Zaidi, mivuto yao huweza kutenga watu wengine au kuwabagua kutoka kwa diskosi ya kijumla kuhusu siasa. Habari za miapango ya makundi yanayoishi katika maeneo yaliyo mbali zinaweza kupatikana katika sehemu ya: Kuwafikia Wafugaji na Makundi Yaliyotengwa.
Wapigakura walio maeneo ya mbali
Katika baadhi ya nchi huenda pia kukawa na Wapigakura walio kwenye maeneo ya mbali. Maeneo haya huwa vigumu kufikia kutumia njia za usafiri, wao huwa vigumu kufikia vyombo vya habari, na maingiliano baina yao na jamii nyingine huwa ngumu. Marekani, jamii kama hiyo huweza kupatikana katika miji kama Alaska, ilhali katika nchi ya Jojia wao hupatikana katika maeneo ya jumla hasa kwenye ukanda wa mlima. Ingawa kuna upungufu wa kufikia maeneo hayo ya mali, huwa kuna nafasi japo kidogo ya kuwafikia chakula na mahitaji mengine. Usafiri kwa helikopta ukipangwa, mipango inaweza kuwekwa kuhakikisha vifaa vya uchaguzi vimewafikia watu. tazama Kuwafikia wafugaji na watu walio mbali na habari hizi.
Walio wachache.
Mipango na taratibu ya awali itahitajika. Vifaa vya upigaji kura lazima viwafikie wanajamii hawa kwa vyovyote vile serikali itaweka mikakati ya kutumia ndege za kwanda na kundi ili kuwafikishia
Jamii huwa hazitoshani. Nchi nyingi zina makundi ya watu walio wachache kwa misingi ya kabila, lugha au utamaduni. Kwa sababu makundi haya ni watu wachache kumekuwepo na mitazamo na tabia ya kuwabagua, ambayo huishia kuwanyanyasa kutojali na utengano na tamaduni tawala unaleta kanuni za kitamaduni na kilugha inayosababisha ugumu wa kuandaa mipango ya elimu ila tu mahusiano ya kimamlaka yakizingatiwa katika maingiliano yao ya jamii kubwa.
Huenda kukawa na pingamizi kwa mipango ya elimu inayoonekana kulenga kulete maridhiano baina ya jamii hizi. Na makundi mengi ya watu walio wachache huenda wakaichukulia demokrasia yeneyewe kama tishio. Kushughulikia tofauti hizi kutoka kwa demokrasia sio jukumu la wakufunzi wa elimu ya uchaguzi pekee yao. Kila mara jambo hilo huwa changamoto kubwa wale walio husika na elimu kwa raia na wenye kushughulikia maendeleo ya demokrasia pamoja na asasi za haki za kibinadamu.
Walemavu
Katika baadhi ya nchi idadi ya watu walemavu na walio na changamoto za kimaumbile inazidi kujipangia mambo yao. Hili ni kweli hasa katika jamii zenye demokrasia ambapo kuna uwezekano wa kufikia rasilimali za kibinafsi na za kiserikali. Kuna lazima ya kuwawezesha watu kushiriki katika uchaguzi na kutowanyima walemavu nafasi ya kupiga kura au kutowapa habari potovu.
Ni vyema kwamba mikakati muhimu na ya kimsingi siyo tu kuhusu elimu kwa walemavu. Habari za kimfumo, na miundo msingi, maendeleo ya methodolojia na kufikia vituo vya kupigia kura, ufunzaji na elimu ya maafisa na wananchi wenye uwezo wa kimwili ni habari muhimu.
Wapigakura walio nyumbani na hospitalini
Kutakuwepo na Wapigakura walio na viunzi au walio wagonjwa na wasioweza kufika wenye vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi. Kwa kutegemea sheria ya uchaguzi na mienendo, mipango inaweza kuwekwa kwa waliozuiliwa nyumbani, au wagonjwa hospitalini, wanaolindwa na wauguzi au walio kwenye vituo vya kurekebisha tabia kuweza kupiga kura. Vituo maalum vianweza kutumia mipango ya upigaji kura kwa wasiokuwepo au kwa kutumia sanduku tamba la kupigia kura. Haya yanaweza kuzingatiwa kupitia mipango ya elimu kwa Wapigakura.
Wafungwa wa jela
Wafungwa hupoteza uhuru wao pindi wanapoamuliwa na korti kwamba wanapaswa kufungwa. Hata hivyo wafungwa huwa hawapotezi uraia wao. Katika baadhi ya nchi kifungo kinaweza kujumlisha kuamua kama haki za kiraia zimenyimwa au la kwa kipindi cha kifungo hicho. Katika nchi nyingine, kuna uchukulio kwamba kupoteza uhuru kunaandamana na kupoteza vitu ambavyo huhitaji uhuru wa kutembea. Upigaji kura huenda ukawa mmoja wao.
Kuongezeka kwa utumizi wa uzuiliaji kwa watu wanaosubiri kifungo, na bado hawajapatikana na hatia yoyote, utumizi wa kifungo kisichohitaji kuzuilia mtu, kupitia kwacho mtu akipatikana na hatia huweza kupiga kura na mwingine aliyezuiliwa kutoweza kupiga kura, jambo hili linadhihirisha kwamba sehemu hii ya watu inahitaji kuangaliwa.
Hali hii hutokea katika jamii zenye kuamini kwamba jela hunuia kuadhibu na kumrekebisha mtu kitabia. Wafungwa hutoka kwenye jela wakati wote na kurejea jamii ya kawaida. Iwapo wanafanya hivyo baada ya kifungo kifupi au kirefu, wanahitaji habari na elimu itakayowawezesha kushiriki kimaendeleo katika jamii. Hili linajumulisha kushiriki katika uchaguzi. Vivyo hivyo, mawazo mengine lazima yaelekezwe kwa elimu ya raia na Wapigakura, iwe kwamba uamuzi uliofanywa unawaruhusu kushiriki katika uchaguzi au la. Mipangilio kama hiyo inatoa changamoto zilizojadiliwa katika sehemu ya Elimu kwa Wafungwa na Elimu kwa Asasi Funge.
Wafungwa wa kisiasa
Katika nchi zinazoendelea na jamii walio katika harakati za mabadiliko huenda kukawa na matumizi mengine ya jela, kama kuzuia wapinzani wa kisiasa na wapinzani wa kijamii. Ama kama bado wako wenye jela au wameachiliwa huru, kama matokeo ya mazungumzo fulani au suluhu la lazima, kuwachwa huru kwa huruma. Kikundi hiki kitakuwa na mahitaji maalum pamoja na kukumbana na changamoto spesheli wanaporudishwa kwenye jamii ya kawaida na maisha ya siasa pamoja na kushiriki katika maendeleo katika siasa na njia nyinginezo. Wafungwa wa kisiasa wasiposhirki katika michakato hiyo, uhalali wa uchaguzi au serikali teule huenda ikatiliwa shaka. Maswala haya yanahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu maalum na unyeti kupitia mipango ya elimu kwa raia.
Maafisa wa usalama
Katika jamii ambazo zimekuwa na ugomvi baina ya raia au mizozo ya ndani, wanachi wanaojumlisha wanajeshi au na polisi huishia kutengwa. Katika hali kama hizi, juhudi maalum lazima ziwe ili kurekebisha tabia. Mara tena, elimu sharti iwafikie wale walio katika kitengo cha usalama na wale walio nje ya kitengo hicho.
Lakini kuna mahitaji mengine ambayo hutokea hata kwenye demokrasia zilizokomaa. Wanajeshi hutumwa kwenye maeneo mageni auyenye kutengwa, maeneo haya yamefungwa kwa athari yoyote ya kijumla ya raia, kwa usalama na sababu za usimamizi, hivyo wanajeshi wanaweza kudhrauliwa. Katika jamii ambazo polisi wamepatiwa nguvu za wanajeshi maswala haya huzingatiwa pia.
Aidha, huduma za kiserikali zenye kutumia nguvu, ama kwa upinzani au ukiukaji au kwa shughuli halali au zisizo halali ya mamlaka ya nchi, hupata lugha, mwendo wa maisha na tamaduni yao wenyewe. Maswala haya yanahitaji kuzingatiwa wakati wa kuandaa mipango ya elimu (tazama, Kuwaendea Wanajeshi na Polisi na Elimu kwa Asasi Funge). Mipango hiyo ya elimu ni muhimu maana maafisa hawa wanaweza kusmamia usalama wa uchaguzi na mabadiliko ya serikali au pingamizi kuu.
Wanawake
Haikubaliwi tena kwa nchi kuweka mifumo ya kidemokrasia na uchaguzi bila kuwapa wanawake uwezo wa kupiga. Uwezo wa kupiga kura kwa wanawake hata hivyo, haukuja bila kupiganiwa. Na haki ya uwezo wa kupiga kura ni kitu kimoja na kuweza kushiriki kikamilifu katika maswala ya raia na kupiga kura katika uchaguzi ni kitu kingine tofauti. Ingawa idadi ya wanawake ni kubwa katika nchi nyingi, mara nyingi wanawake huwa wamewakilishwa kwa kiasi kidogo sana katika siasa.
Elimu pekee yake haitabadilisha hili. Lakini kuna uwezekano wa kutayarisha mipango ya elimu itakayoshughulikia vizingiti vya kitamaduni na kiuchumi vinavyoathiri wanawake katika kushiriki kwao. Kuna mifano ya vifaa vilivyobuniwa kutimiza mahitaji ya kihabari na kielimu ya wanawake ulimwenguni wote.
Wapigakura Vijana na Wapigakura wa mara ya kwanza
Katika kila uchaguzi huwa kuna Wapigakura wapya ambao wamefikisha umri wa kupiga kura. Mipango katika shule huishia kuwahimiza Wapigakura vijana kurhsiriki katika uchaguzi. Lakini elimu ya ziada kwa Wapigakura inahitaji kutayarishwa as inayoakisi utamaduni wa vijana. Jambo hili hutendeka sana katika nchi zinazoendelea na kwa jamii zilizokatika mabadiliko ambapo idadi ya vijana ni kubwa na mahali ambapo vijana huhamasishwa kuunga mkono chama kimoja au kingine wana watu ambao hata hawana maono yoyote kwa vijana.
Mwananchi yeyote anyepiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mara nyingi atakuwa na habari ndogo kuhusu haki zake na kuhusu mchakato wa uchaguzi. Wapigakura wa mara ya kwanza huenda wakapata kuwa baadhi ya michakato ya usajili na upigaji kura kuwa na umangimeza mwingi na wakati mwingi kutisha. Waelimishaji sharti watambue habari hitajika na pengine woga wa kikundi hiki ili kuhakikisha kwamba mambo haya yanaweza kuepukwa ili kundi hili lisijiondoe katika mchakato wa uchaguzi.