Pamoja na mahitaji ya kielimu ya Wapigakura kwa jumla na makundi mengine lengwa, kutakuwa na mazingatio mengine ambayo lazima yashughulikiwe.
Mazingatio ya Kisiasa, Kikatiba na Kisheria:
Katiba na sheria inaweza kuweka mazingatio mengine kwa waelimishaji hasa kutoka kwa mamlaka ya uchaguzi, mashirika ya kiserikali inapofikia habari na elimu kwa Wapigakura. Watahitajika kutoa habari kwa Wapigakura kwa ujumla na au kwa makundi mahususi katika jamii. Shinikizo la kisiasa linaweza pia kuathiri mahusiko ya mipango ya elimu kwa Wapigakura.
Mazingatio ya vifaa:
Mazingatio mengine huweza kujitokeza. Kwa mfano, kunayo makundi mengine katika maeneo ya mbali, ambayo yatahitaji kufikiwa? Miundo msingi ya uchukuzi na mawasiliano ina matatizo. Vizingiti hivi vya vifaa ni vya halali au ni vya kuwekwa ili kuzuia watu wengine kupata habari? Vizingiti hivi vya vifaa vinaweza kuepukwa na ni rasilimali zipi zinazohitajika? Majibu ya maswali haya yataathiri mipango ya elimu ya uchaguzi.
Maadili ya Waelimishaji:
Mwisho, waelimishaji huletamaadili yao binafasi katika shughuli ya elimu kwa Wapigakura. Wao huleta michukulio na mapendeleo yao. Mambo haya yanahitaji kushughulikiwa ili kuhakikisha kwamba mipangio ya elimu inashughulikia mahitaji ya Wapigakura badala ya kutimiza matakwa ya wasomi.