Wakati itakapokuwa rahisi tu kutumia njia za kibunifu na kivumbuzi kutoa elimu ya uchaguzi na suluhisho linaloshughulikia Wapigakura wote kupata suluhu mwafaka humaanisha kupata ulinganifu baina ya wazo lenyewe na utekelezaji wake. Lakini pia huenda hakuna uwezekano huo. Na itabidi uchaguzi ufanywe kwa misingi ya vikwazo vilivyopo. Miongoni mwa vikwazo hivi ni kama vile:
- Ukubwa wa makundi fulani
- Kutenga makundi fulani
- Uwezo wa kupata vifaa vilivyochapishwa au vilivyotafsiriwa
- Muda uliopo
- Uwezo wa kusafirisha na kusambaza vifaa
- Idadi ya waelimishaji waliopo
Kutokana na bajeti finyu pamoja na uchaguzi wa kuendeshwa, kuna uwezekano kwamba mipango ya elimu itakuwa na upungufu. Lakini itakuwa muhimu kwa waelimishaji kutia juhudi za kupunguza, kuondoa vikwazo kwenye mipango.
Kwa sababu lazima pawepo na vituo vya kupigia kura, hata katika maeneo mbali na kwa sababu maeneo hayo yatahitaji vifaa pamoja na maafisa wa uchaguzi, waelimishaji wa Wapigakura wataweza kufikia maeneio hayo. Muhimu zaidi, mipango bora inaweza kupunguza vikwazo na kufahamishwa kuhusu saa na mahali pa kupigia kura, hivyo watakuja na utambulisho, watajua jinsi ya kutia alama kwenye karatasi ya kupiga kura, na wataweza kupitia taratibu ya upigaji kura bila matatizo, hivyo kupunguza idadi ya wafanyikazi wanaohitajika katika vituo vya kupiga kura na vile vile kupunguza maafisa wa usalama.
Mijada hii yenye kupendelea elimu ya uchaguzi licha ya vikwazo vya vifaa inapendekeza wanaoweka vikwazo vya vifaa wanapaswa kuchunguzwa ili kuhakikisha kwamba hawafanyi hivyo ili kuzuia makundi ya Wapigakura kuafikia upigaji kura. Hata hivyo kuna wakati ambapo waelimishaji watalazimika kutathmini gharama na manufaa na kukubali kuwa kuna Wapigakura wengine ambao wamebaguliwa katika mchakato mzima.