Kuuliza maswali yaliyowahi kuulizwa kwingineko pia husaidia kulinganisha matokeo ya mtu huyo na yale ambayo yamepatikana katika maeneo mengine na katika nyakati nyingine. Hili ni muhimu. Matokeo yoyote yale kutoka kwenye uchunguzi – kama vile kwamba 34% ya Afrika Kusini hawana nia katika siasa – inaweza kumaanisha mengi katika hali hiyo. Kwa upande mwingine, inaweza kumaanisha zaidi tukijua kuwa ilikuwa juu kabisa, chini kabisa, au sawa na ya watu katika nchi nyingine.
Vile vile, muktadha fulani unaweza kuhitaji swali lililo na upekee katika msuko wake. hivyo basi, kuna tofauti ya wazi katika ya kujenga maswali ambayo yanafaa tu katika muktadha maalumu, na kutoa matokeo ambayo yakiulinganishwa yanasaidia kuimarisha uelewa wa mielekeo mbalimbali ya eneo husika. Zaidi ya kauli hizi zote za kijumla, kuna uwezekano wa kuwa na mitego ya kisiri ambayo mtungaji wa swali hilo hana budi kuitambua.
Maswali wazi
Maswali haya humruhusu anayejibu kuyajibu moja kwa moja, katika kauli zao wenyewe. Badala ya kuwauliza watu kukudiria umuhimu wa sababu mbalimbali za kupiga kura kwenye kipimo “muhimu sana” hadi kwa “si muhimu kabisa” kwa mfano, mtu anaweza kuwauliza: “Ni sababu zipi muhimu hasa za kupiga kura?” Hivyo, watakuwa na nafasi ya kutolazimika kurudia kinachohitajika kuthibitishwa.
Maswali wazi hata hivyo, ni ghali sana. Makampuni mengi ya uchunguzi huruhusu uwepo wa maswali matatu au manne hivi pekee. Swali la sampuli hiyo, kama vile “Ni matatizo yapi muhimu yanayoikabili nchi?”, yanaweza kupata majibu mengi zaidi ya kipekee. Yote yanapaswa kuulizwa na kuwekwa katika makundi au “kupangwa” katika makundi makubwa yanayochukuliwa kuwa muhimu. Shughuli hii inagharimu muda mwingi sana na gharama yake ya utendakazi huwa juu sana.
Maswali funge, yale ambayo yanaelekea kuwa na majibu funge ambayo watu wanaweza kuchagua tu yale ya kujibu, pia yanatokeza matatizo mengi ambayo yanajadiliwa katika maelezo ya kina yaliyopo hapo chini.
Mpangilio
Upangaji unarejelea jinsi maswala muhimu yanavyowasilishwa au “kupangwa” katika swali la uchunguzi. Ni sehemu gani za suala pana zinazopaswa kunaswa? Ni kundi gani la sera mbadala zinazopaswa kutolewa kwa watakaojibu? Je, swali kuhusu eneo la bunge linapaswa kugusia gharama na ustahifu? Je, Afrika Kusini iwe na mji mkuu mmoja wa usimamizi katika Pretoria, kwa mfano, na mwingine mmoja wa kutunga sheria katika Mji wa Cape. Au je, ziwekwe zote mbili katika mji mmoja? Au, swali liulize kuhusu kubadilisha hali iliyopo? Pia, kama mfano, je, bunge libaki katika Mji wa Cape, pale lilipo hivi sasa, au lihamishiwe Pretoria au kwingineko? Maswali haya yanaweza kuvutia majibu tofauti kabisa, na athari tofauti tofauti za kisiasa.
Japo maumbo tofauti tofauti yanaweza kusababisha matokeo tofauti tofauti, ni vigumu kufanya maamuzi kuhusu mifumo ya kutumia na mara nyingi yatachochea uhakiki kutoka kwa makundi fulani ya kisiasa.
Mpangilio wa Maswali
Mpangilio wa maswali unaweza kuathiri majibu kwa kubadilisha muktadha mkubwa ambamo wanaojibu wanafikiria kuhusu suala. Kwa kuwa majibu ya swali moja yanaweza kuathiriwa na majibu yaliyotolewa kabla, maswali ambayo kwa kiwango kikubwa hayaegemei upande wowote yanaweza kusababisha athari tofauti kabisa yakiulizwa pamoja na mengine. Maswali kuhusu uwezekano wa kujitokeza kwa wapigakura, kwa mfano, yanaweza kuegemea upande wa viwango vya juu vya ushiriki ikiwa maswali hayo yalitanguliwa na na vipengele vinavyowauliza watu kuhusu wajibu wa watu wa kupiga kura, hivyo basi kuwakumbusha kuhusu wajibu huo wao.
Mpangilio wa Majibu
Mpangilio ambamo majibu yatakayopatikana yataorodheshwa unaweza pia kuwa na athari muhimu kwa matokeo. Iwapo majibu yenye misimamo mikali yanawekwa kabla ya majibu yenye mwelekeo sawazishi – athari “kinzani”- majibu hayo yaliyotangulia yenye misimamo mikali huzidisha uwezekano wa kuchagua majibu yafuatayo yaliyo sawazishi.
Athari za kimpangilio pia hutofautiana kulingana na mbinu ya mahojiano. Kutokana na chunguzi za simu na mahojiano ya moja kwa moja zinazosomwa, kuna “athari ya usasa” ambapo wanaojibu huelekea huchagua vibadala vya siku za karibuni kutoka kwenye orodha kwa sababu wana wakati wa kutosha kufikiria kuyahusu. Tofauti na haya, mawasilisho ya picha kama vile kadi onyeshi au hojaji za kutumwa kwa njia ya barua pepe inaweza kuwa “athari ya ghafla au ya kimlipuko” ambapo vibadala vya awali huteuliwa kwa sababu kwa kiwango kikubwa watu watafikiria kuhusu kibadala cha kwanza.
Maswali ya upande mmoja dhidi ya Yale kulazimishiwa Jibu
Maswali ya “kuegemea upande mmoja” huwauliza watu kukubali au kukataa kwa kutoa kauli, kupendelea ua kupinga msimamo mwingine, au kutaja sehemu fulani ya kiwango cha maoni. Kukiwa na maswali ya “kulazimishiwa jibu”, mtafiti hujaribu kutoa vibadala sawazishi, kama vile, “Je, unapendelea serikali kutekeleza sera X, au itekeleze sera Y?”
Majibu ya “kukubali” au “kutokubali” huelekea kuegemeza matokeo kwa jibu “kubali”, hasa ikiwa elimu kuhusu jambo ni finyu. Wanaojibu ambao viwango vyao vya elimu na uzoefu wa kisiasa ni vya chini ndio wanaoweza kuathirika sana na athari hii. Iwapo watu hawajafikiria kuihusu mada kwa kina, huenda wakakosa kuzua mijadala ya kupinga kauli za kuegemea upande mmoja na huenda wakakubali.
Suluhisho bora litakuwa kuwapa wanaojibu kibadala bora cha pili, au hata cha tatu – chaguo la kulazimishiwa. Hili huwapa wanaojibu mtazamo mwingine kuhusiana na mjadala huo. Hili kwa jumla hupunguza idadi ya watu wanaopendelea mfumo wa upande mmoja na pia hubadilisha mpangilio wa maoni. Ingawa uzito wa hoja zote na vibadala vyote vya majibu vinavyowasilishwa ni muhimu – vyote haviwezi kutoshana kwa viwango vya ubora. Kuetengeneza kibadala cha pili pia huwaweka watafiti katika nafasi mbaya ya kuathiri msuko wa maoni ya umma kwa kuamua vibadala vinavyoweza kujumuishwa humo na vilevile yaliyomo katika vibadala hivyo.
Maswali yenye ncha Mbili
Mtego mmoja unaopaswa kuepukwa ni swali lenye ncha mbili. Hapa kibadala kinachopendekezwa hufungamanishwa na suluhisho lake. Mfano unaweza kuwa, “Je, unaruhusu kuongezwa kwa ushuru ili kupunguza upungufu kwenye bejeti?” Wanaojibu huenda wakakosa kuwa wazi kuhusu jibu lao linavyopaswa kumaanisha.
Je, “ndiyo” inamaanisha umekubali kuongezwa kwa ushuru, kwa mfano, au kutupilia mbali upungufu huo, au vyote viwili?
“Swali lenye ncha moja na nusu” hujumuisha mahitaji yanayowaongoza wanaojibu katika kuchagua kibadala mwafaka.
Maneno Muhimu
Sehemu nyingine inayoweza kuwa na ugumu ni maneno halisi yanayotumiwa kueleza kitu hicho au kurejelea pendekezo fulani. Je, ufadhili wa serikali umeratibiwa kukabiliana na “uraibu wa kutumia dawa” au “kuwakomboa watu kutokana na utumizi dawa wa dawa za kulevya”, “usaidizi kwa maskini” au “maslahi,” au “kuimarisha hali ya maisha ya watu maskini”? Je, wanaojibu wanaulizwa kukubali “sera ya rais” au jinsi “anavyoishughulikia sera hiyo”?
Ni maneno gani yanayofafanua chaguo halisi ambalo wanaojibu wanatakiwa kufanya? Je, wanatakiwa “kukubali,” “kuunga mkono,” au “kupendelea” kitu fulani, au kukitazama kama “bora zaidi,” bora,” “kiwango cha haja tu” au “kibaya”?
Umbo jingine maalumu la tatizo hili ni kuhusisha maneno ya “uvumi”, au maneno yanayotumiwa kuchochea majibu ya hasira kutoka kwa wanaojibu, walio na vibadala vya majibu. Maneno haya yanaweza kuchochea teuzi za kupendelea upande mmoja au za kimitazamo katika majibu yao, na vilevile kufungua mwanya wa kuingia kwa majibu yasiyo ya kitaalamu. Katika Marekani, neno “mkomunisti” lilijulikana sana kutokana na athari yake kwa majibu yaliyotolewa kuhusu sera ya maswala ya nje. Mtajo wa rais mara nyingi huwa na athari kwenye matokeo, hasa ya kupendelea yale ambayo ikulu imefanya. Katika Afrika Kusini, mtu anaweza pia kupata matokeo tofauti ikiwa watu wanaulizwa kulinganisha maisha yao ya sasa na miaka ishirini iliyopita, yaani, wangeulizwa kulinganisha na maisha yao “chini ya siasa za ubaguzi kwa misingi ya rangi.”
“Wale Wasiojua”
Muundo wa swali pia huathiri idadi ya watu wanaotoa maoni. Idadi kubwa ya “wale wasiojua” (DK) hupatikana kutokana na maswali ya ninakubali/ninakataa, maswali kuhusu masuala ya kizamani na yale ya kidhahania, na yale ambayo yalikuwa na jukumu gumu awali (k.m., yale yanayohitaji maelezo marefu au yanayohitaji wanaojibu kukadiria mbali)
Kiwango cha utojua, DK, kinaweza pia kuathiriwa na matumizi ya “chujio”, kama vile, “Au hujawahi kuwa na nafasi ya kufikiria kuhusu hili?” Chujio mara nyingi huongeza idadi ya majibu ya watojua, DK, hivyo basi kuhalalisha Utojibu. Hata hivyo chujio pia zinaweza kuathiri usambaaji wa maoni. Wale ambao huenda wakatoa maoni hata ingawa hawakuwa nayo hawatoki katika makundi mbalimbali yaliyopaswa kujibu bila mwelekeo maalumu. Tatizo hilo huzidishwa na “wale wasio na msimamo maalumu” (wale wanaotoa majibu tofauti tofauti kwa aina na miundo mbalimbali ya maswali) huwa vigumu kuwakadiria na hawadhihiriki kuwa na sifa moja.
Ugumu wote unaorejelewa katika sehemu hii hutokea kwa sababu ya jinsi binadamu wanavyofikiria. Jinsi binadamu wanavyofasiri habari huathiriwa zaidi na jinsi habari hiyo inavyowasilishwa. Hii ni kweli kwa mazingira ya uchunguzi. Watu hawafanyi chunguzi kamili kwa masuala wakilishi ya maoni au mielekeo katika kumbukumbu za muda mrefu. Badala yake, wao hutafuta habari inayopatikana ama kutoka katika miktadha ya mazingira yao katika siku za hivyo karibuni au uzoefu, au kutoka kwenye muktadha wa karibu wa hojaji na mahojiano.
Hakuna majibu rahisi. Maana ya swali mara kwa mara hutegemea kwa kiwango fulani mahali linakowekwa katika hojaji. Jinsi tunavyolichukulia jibu letu mara kwa mara hutegemea kwa kiwango fulani vibadala vya majibu na jinsi tulivyowasilishiwa.
Kando na “kanuni chache za ishara ya kidole” zilizokubaliwa, hivyo basi, hakuonekani kuwa na masuluhisho ya moja kwa moja kwa matatizo ya wingi wa maneno. Japo tunaweza kujaribu kuepuka maswali “chafuzi”, maswali “safi” yaliyotolewa katika muktadha wa kisiasa huenda yakakosa ukweli au yakawa yasiyofaa. Uvumi na mahusiano yenye ncha mbili ndiyo mara nyingi yanayoyapa maswali ya uchunguzi uhalisia wa kisiasa.