ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Kolumbia ya Uingerea: Ushiriki Dhabiti wa Raia

 

 

Serikali ya Mkoa wa Kanada wa Kolumbia ya Uingereza, kwa kuidhinisha kikamilifu Bunge la mkoa huo, limeanzisha mchakato wa kihistoria, pekee na ongozi katika mageuzi ya uchaguzi kwa kubuni Bunge la Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Uchaguzi. Hii ndiyo mara ya kwanza ambapo serikali imelipa kundi la raia walioteuliwa bila kanuni maalumu fursa na jukumu la kurekebisha kivyao mfumo wa uchaguzi na kuhakikisha kwamba mapendekezo yao yanawasilishwa kwa umma ili kuidhinishwa katika kura ya maamuzi.   

Uchaguzi wa mwaka 1996 bunge la mkoa wa Kolumbia ya Uingereza ulifanywa chini ya mfumo wa FPTP. Uliishia katika NDP, na asilimia 39 ya wingi wa kura, kushinda viti 39 katika Bunge Kuu – zaidi ya viti 33 vya Chama cha Liberal, ambacho kilikuwa kimeshinda asilimia 42 ya wingi wa kura. NDP, kilichokuwa na wafuasi wachache kushinda Chama cha Liberal, hivyo basi kilibuni serikali kwa miaka mitano baadaye. Matokeo haya yalikichochea Chama cha Liberal kuyatilia maanani mabadiliko katika kampeni zake za kisiasa kwa uchaguzi ujao. Katika uchaguzi wa mwaka 2001 ambapo Chama cha Liberal kiliahidi kutekeleza mabadiliko ya uchaguzi kupitia kwa Bunge la Wananchi: kufuatia ushindi wa uchaguzi uliotoa asilimia 97 ya viti bungeni kutokana na asilimia 58 ya wingi wa wapigakura, ilikuwa na mamlaka ya kutekeleza maazimio haya.        

Mfano mmoja wa mwelekeo ulitumiwa nchini Kanada kwa ujenzi wa maswala ya sera ya umma ambapo serikali inatafuta maoni ya umma ni kubuni tume au bodi ya uchunguzi wa umma, hasa inayoongozwa na majaji, wataalamu au viongozi wa kisiasa. Baada ya kukaribisha maoni ya umma, na baada ya muda majadiliano mengi, serikali hufanya uamuzi kuhusu hatua zitakazofuata, kwa kuzingatia ripoti iliyotolewa na tume.   

Mpango wa Bunge la Wananchi na mpangilio wa shughuli zake vilitayarishwa na Gordon Gibson, na mwandishi mwingine kuhusu demokrasia na aliyekuwa kiongozi wa chama cha kisiasa kuhusu shughuli na maswala ya umma, na serikali mpya kwa ushiriano na wataalamu wa kurekebisha uchaguzi. Kulikuwa na sifa mbili za kipekee za Kolumbia ya Uingereza: watu walioteuliwa wasingekuwa wataalamu katika uwanja wa kurekebisha uchaguzi, lakini wangekuwa raia waliochaguliwa bila mpangilio maalumu kutoka katika mkoa mzima; na, ikiwa mabadiliko yoyote yangependekezwa, swali lingependekezwa moja kwa moja kwa raia wa mkoa huo katika kura ya maamuzi na lisingelazimishwa kuingia katika serikali.   

Bunge la Wananchi lililoibuka kutokana lilijumuisha wanaume na wanawake 160 waliokuwa huru na wasio na mapendeleo katika umri wote katika mkoa wote wa Kolumbia ya Uingereza, iliyochaguliwa bila mpangilio maalumu kutoka kwenye rejista ya uchaguzi. Awamu ya uteuzi iliratibiwa kusawazisha orodha ya wanaume na wanawake, kwa kuzingatia umri wao katika mkoa huo wa Kolumbia ya Uingereza ilivyoripotiwa katika hesabu ya idadi ya watu ya mwaka 2001, ikiwa ni pamoja na watu wawili kutoka kwenye jumuiya aboriji, na kuwakilisha mkoa mzima. Hii ilifuatiwa na awamu ya mafunzo kwa Bunge ambapo wataalamu wengi wa mfumo wa uchaguzi walitoa nyenzo za kusoma (zilizokuwepo pia kwa umma) na kufaya vikao na raia ili kuwaarifu kuhusu mifumo tofauti iliyokuwepo na kujadili manufaa na ubaya wake.

Mwishoni mwa ripoti ya awamu ya mfunzo, Kauli Funguzi kwa watu wa Kolumbia ya Uingereza, ilitumwa kwa makundi mbalimbali katika jamii, wakiwa pamoja na Bunge, maktaba, ofisi za manispaa wilayani, shule na vyuo vikuu, ili kuuarifu umma kuhusu miafaka ya Bunge la Wananchi. Ripoti hii ilifuatiwa na awamu ya vikao vya umma, ambapo takribani watu 3000 walihudhuria vikao vingine 50 vilivyofanywa katika sehemu zote za mkoa. Katika awamu zilizofuata za kutekeleza, vikao na makundi ya kujadili vilifanyika ambapo Bunge lilipunguza uteuzi wa mifumo ya uchaguzi hadi kwa miwili na, kama kundi ikaeleza kwa kina kila mfumo. Siku ya kwanza ya awamu hiyo ilikuwa na kurudiwa kwa mawasilisho bora yaliyosikika wakati wa vikao vya umma- mawasilisho yaliyotetea mifumo mbalimbali ya uchaguzi na sifa zake. Malengo ya awamu hizi zote yalikuwa kutambua vipengele muhimu vilivyohitajika kwa mfumo wa uchaguzi katika Kolumbia ya Uingereza, kupitia vilivyo aina zote za mifumo ya uchaguzi kuhusiana na vipengele hivi na, hasa, kuongeza ufahamu, ushiriki na kujumuishwa kwa umma. Vipengele vitatu muhimu vilivyoafikiwa mwishoni vilikuwa uteuzi wa wapigakura, uwakilishi kimaeneo na usawa. Mwisho, mwishoni mwa Oktoba mwaka wa 2004, Bunge liliwasilisha pendekezo lake, ambamo liliunga mkono (huku watu 146 wakiunga na saba kupinga), dhidi ya kubadilisha mfumo wa FPTP hadi kwa ule wa STV. Kukamilika kwa mchakato wa Bunge la Wananchi hivyo basi ulihitaji chapisho la ripoti ya mwisho rasmi na kuwasilisha mapendekezo hayo katika kura ya maamuzi.   

Mfumo huu shirikishi ulivutia ari ya makundi mengi katika nchi nzima ya Kanada. Suala hilo lilipendekezwa kwa serikali nyingine nchini Kanada kama njia nzuri ya kuwahusisha wananchi katika masuala yanayopaswa kujulikana na umma, na mchakato kama huo kwenye ule ulioko Kolumbia ya Uingereza ulianzishwa na serikali ya Ontario.  

Chaguzi nyingine nchini Kanada pia zimechangia katika kuimarika kwa uungwaji mkono wa mabadiliko katika mchakato wa uchaguzi. Serikali nyingi za miungano mara nyingi zimechaguliwa na chini ya asilimia 50 ya kura. Kwa sababu hii, hatua mbalimbali za mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi katika kiwango cha jimbo, ikiwa ni pamoja na Kura Huru nchini Kanada (FVC), zimejitokeza, sawa na walivyojitokeza watetezi wengi wa haki.

Kuna sababu ya kufikiria kuwa yaliyofanyika katika Bunge la Wananchi nchini Kolumbia ya Uingereza yatakuwa na athari fulani kwenye mijadala ya baadaye kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, na kuhusu mchakato wa kurekebisha na kubadilisha hasa, katika kiwango cha jimbo nchini Kanada. Kutokana na shinikizo kutoka kwa NDP na Chama cha Conservative, marekebisho yafuatayo kwenye Hotuba kutoka Ikulu yalikubaliwa kwa kauli moja katika mwezi wa Oktoba mwaka wa 2004: ‘Kauli ya Marejeleo kwenye Kamati Kuu kuhusu Hatua na Masuala ya Ndani ikiiagiza kamati kupendekeza mchakato ambao ungewahisisha raia na wabunge katika kuchunguza mfumo wetu wa uchaguzi wakirejelea vipengele vyote’.

Hatua ya baadaye ya Bunge la Wananchi nchini Kolumbia ya Uingereza kuhusu mchakato wa marekebisho na mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi kwa kiwango cha kimataifa haijadhihirika wazi, ingawa ni bora kusema kwamba ujenzi wake na kazi yake vimeimarisha ari ya watu ndani yake kuzidisha ufahamu wa michakato shirikishi duniani kote.