ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Chile: Mfumo Uliotatizwa na Nia za Wasomi

Mfumo wa uchaguzi wa Chile unaweza kueleweka tu katika muktadha wa kipindi kirefu cha uongozi wa kiimla chini Jenerali Augusto Pinochet (1973-90), ambao lengo lake lilikuwa kubuni mfumo demokrasia iliyolindwa, ya kiimla, ambao mfumo wa uchaguzi ulikuwa sehemu yake. Udikteta uliondoa mfumo wa PR, ambao ulikuwa katika matumizi kabla ya mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 11 Septemba, 1973. Mfumo wa PR ndio uliokuwa jibu la mianya katika muundo wa kijamii wa Chile tangu karne ya 19 na ulikuwa umeanzisha mfumo wa vyama vingi. Kufikia miaka ya 1960 hivi vilikuwa vimeungana katika vyama sita vikuu – viwili kwenye mrengo wa kushoto (Wasosholisti na Wakomunisti), viwili katika mrengo wa kati (Wanademokrasia wa Kikristo na Radikali), na vingine viwili kwenye mrengo wa kulia (Liberals na Conservatives, vilivyoungana katika mwaka 1966 kujenga Chama cha Taifa, NP).

 Mfumo wa Vipeo: Hiba ya Udikteta

 

Katika mipangilio ya kikatiba ya mabunge mawili nchini Chile, Kitengo cha Manaibu, bunge la chini, linajumuisha wanachama 120 waliochaguliwa kwa kipindi cha miaka minne, wawili kwa kila wilaya 60 za uchaguzi. Seneti ina wanachama 38, wawili kwa kila wilaya 19, waliochaguliwa kwa kipindi cha miaka minane: kuna chaguzi kwa nusu ya viti kila miaka minne, sambamba na chaguzi za Kitengo cha Manaibu. Kuna wanachama tisa wasiochaguliwa, maseneta wa ‘taasisi’ au ‘walioteuliwa’, waliotangazwa na Baraza la Kitaifa la Usalama (wanne), Mahakama ya Juu (watatu) na rais (wawili), na mwanachama mmoja mwenye cheo maalumu, aliyekuwa rais Eduardo Frei Ruiz-Tagle. (Maeneo 13 asilia ya useneta kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1980 yalipanuliwa hadi 10 katika marekebisho ya katiba ya mwaka 1989 ili kupunguza mamlaka ya maseneta wasiochaguliwa). Utaratibu huu ulijadiliwa na Pinochet na wafuasi wake walipotoka mamlakani katika hatua ya kuingia kwenye demokrasia.   

Vyama, miungano au wagombea huru huwasilisha orodha, aghalabu zilizo na wagombea wawili kwa kila wilaya, katika uchaguzi kwa Bunge la Manaibu na Seneti. Wapigakura humpiga kura mgombea wa hiari yao. Kiti cha kwanza huendea orodha yoyote inayopata idadi kubwa ya kura kwa jumla: mjumbe aliyechaguliwa ni mgombea aliye kwenye orodha hiyo anayepata kura nyingi. Ili kuchukua viti vyote viwili, orodha inayofaulu kabisa inapaswa kupata mara mbili ya idadi ya kura za orodha ya pili. Mfumo huu hulazimisha vyama kujenga miungano ya uchaguzi kwa sababu hatua inayohitajika iko juu: asilimia 33.4 ya jumla ya kura zilizopigwa kwa orodha ongozi huhitajika ili kushinda kiti kimoja. Hata hivyo, orodha huhitajika kupata asilimia 66.7 ya jumla ya kura zilizopigwa ili kupata viti vyote viwili.  

Kuna miungano miwili mikuu ya uchaguzi, ambayo katika mwaka wa 2001 ilishinda viti katika Bunge la Manaibu ila kimoja. Concertación por la Democracia hubuniwa na vyama vinne vinavyopinga utawala wa Pinochet (Wasosholisti, Chama cha demokrasia, Wanademokrasia na Waradikali) na kiliongoza kutoka kurudi kwa demokrasia katika mwezi wa Machi katika mwaka wa 1990 hadii Machi 2010. Muungano wa mrengo wa kushoto nchini Chile (Muungano Huru wa Huru, UDI, na National Renewal, RN) uliunga mkono utawala wa Pinochet. Orodha ya Concertación inajumuisha mgombea mmoja kutoka kila mojawapo wa makundi mawili yaliyo katika muungano, yaani, mmoja kutoka Wanademokrasia wa Kikristo na mwingine kutoka kwa Wasosholisti, Chama cha Demokrasia na Waradikali. Hakuna eneo ambalo lina ushindani kati ya Wasosholisti na Chama cha Demokrasia. Kwenye orodha ya upinzani, UDI na National Renewal aghalabu huwasilisha mwanachama mmoja katika maeneo yote.

Matokeo ya mfumo huu wa uchaguzi ni kwamba takribani maeneo yote hurudisha mwakilishi mmoja kutoka kwenye Concertación na mmoja kutoka kwenye Muungano wa Chile. Mfumo huo ungejenga  ushindani kati ya wagombea wawili kwenye orodha hii kwa kiti kimoja itakachoshinda, lakini kwa kawaida hili hufungiwa katika kuwajumuisha wasomi kwenye miungano.

Mfumo huu wa uchaguzi una upekee kwa sababu kwa kawaida hupendelea wafuasi wachache, bali si wengi. Kwa hivyo si mfumo wa ungiwatu. Ni mfumo unaotyumia mbinu ya usawa,lakini matokeo, japo matokeo yake hukosa usawa, kwa kuwa huiruhusu orodha ya uchaguzi kuchukua nusu ya viti kwa asilimia 34 tu ya kura. Sababu ya pekee ya kutokafanyika kwa uharibifu huu ni mipaka ya ushindani wa kisiasa.   

 Mfumo wa uchaguzi ulibuniwa na utawala wa kijeshi kufuatia kura ya maoni ya tarehe 5 mwezi wa Oktoba 1988. Kura hiyo ya maoni ilikuwa na malengo mawili: kuimarisha katiba ya mwaka 1980 na kuchagua Jenerali Pinochet kwa miaka mingine minane. Katika uchaguzi uliokosa ushindani (hakukuwa na mgombea mwingine), Pinochet alishindwa na Concertación. Hili lilichochea mabadiliko ya kuingia katika demokrasia, na chaguzi za kongresi na urais za mwaka wa 1989, uchaguzi wa urais ukishindwa na mgombea wa upinzani Patricio Aylwin (Mwanademokrasia wa Kikristo). Mfumo wa uchaguzi uliratibiwa kutetea vyama viwili vya mrengo wa kulia, ambavyo vilikuwa vimeunga mkono ugombea wa Pinochet, huku ikiwa wazi kwamba ushindi katika kwa wasindani wao. 

 Katika chaguzi tatu za urais na kongresi zilizofanyika kati ya mwaka 1990 na 2000, Concertación kimepokea kura nyingi, japo hakijawahi kuongoza Seneti kwa sababu maseneta wengi wa kiasasi huunga mkono upinzani.

Matatizo ya Mfumo Vipeo kwa Vyama na Kwa Demokrasia

 

Upinzani mwingi umetokezwa dhidi ya mfumo wa uchaguzi. Kwanza, hulazimisha vyama kuingia katika miungano kwa sababu ya idadi kubwa ya kura inayohitajika kushinda uchaguzi. Pili, una athari hasi kwenye uwakilishi kwa sababu umeweka Chama cha Kikomunisti nje ya Kongresi, licha ya umuhimu wake hadi mwaka wa 1973 na asilimia 5-7 ya kura kitaifa katika demokrasia mpya. Tatu, kwa kila muungano kwa kawaida utashinda kiti kimoja, ushindani mkubwa hufanyika miongoni mwa vyama vishiriki, badala ya kati ya miungano na vyama pinzani. Mivutano hii huhatarisha udhabiti wa mgombea mmoja katika maeneo saba katika hayo tisa, au kuweka mgombea hafifu ambaye hatatatiza mgombea wa kuongoza. Nne, mfumo huo huweka mamlaka makubwa mikononi mwa viongozi wa chama, ambao huchagua washindi wakiunda orodha hizi. Kukikosekana ushindani wa kweli katika maeneo mengi, wapigakura hukosa ari katika chaguzi, na hata zaidi kama hakuna mgombea wa chama chao wa kupigia kura.       

Upungufu huo umeishia serikali katika kupendekeza kwamba kuwe na mabadiliko ya uchaguzi na kupendekeza kwamba, badala ya maeneo ya wagombea wawili, maeneo mapana yanaweza kutoa matokeo mengi yenye usawa yatafaa. Hili halijapenya, hata hivyo, kwa kuwa vyama vya Concertación huogopa wasichokijua, na upinzani hutetea mfumo uliopo kwa sababu ya upeo mzuri wanaopata.

Chaguzi za Urais

 

Katiba ya mwaka 1980 inaweza mfumo wa awamu mbili kwa chaguzi za urais. Idadi kubwa ya kura inahitajika kwa ushindi katika awamu ya kwanza, huku kukiwa na nafasi ya kura za awamu ya pili hili likikosa kufanyika. Asasi hiyo ya upigaji kura huelekea kuimarisha siasa za miungano. Washindi wa chaguzi za urais katika miaka ya 1989 na 1993 - Patricio Aylwin wa na Eduardo Frei Wanademokrasia wa Kikristo, mtawalio – walichaguliwa kwa wingi wa kura, ingawa katika mwaka wa 1999 kulikuwa na kura chache tu 30,000- tofauti ya kura kati ya Ricardo Lagos na mpinzani wake wa mrengo wa kulia, Joaquín Lavín. Lagos alishinda kwa asilimia 50.27 ya kura katika awamu ya pili. (Chini ya katiba ya kitambo (ya 1925), ambapo hakuna mgombea aliyeshinda urais, ilivyofanyika katika miaka ya 1946, 1958 na 1970. Katika kila kisa ulichagua mgombea aliyekuwa na kura nyingi.)

Usajili na Upigaji Kura: Wa Kujitolea au wa Lazima

 

 Tatizo jingine lililoonekana kuwapo katika mfumo wa uchaguzi ni kwamba usajili ni wa kujitolea lakini upigaji kura ni wa lazima. Rejista mpya za uchaguzi zilifunguliwa katika mwezi wa Februari mwaka 1987, pale ambapo utawala wa kijeshi ulikuwa ukijiandaa kwa kura ya maoni ya Oktoba mwaka 1988, rejista za kitambo zilikuwa zimechomwa na majeshi mwaka 1973. Upinzani wa kidemokrasia ulitafuta uungwaji mkono ili kupata wapigakura waliosajiliwa; mkakati wake ukiwa kumshinda Pinochet katika uchaguzi ili kuafikia demokrasia, na ulifaulu kwa kupata asilimia 92 ya wapigakura halali kujisajili. Tangu wakati huo, hata hivyo, idadi ya wapigakura waliosajiliwa haijaongezeka kulingana na idadi ya umri wa kupiga kura, kwa kuwa vijana sasa hivi hawatilii maanani kushiriki katika uchaguzi. Katika chaguzi za kongresi za mwaka 2001 asilimia 80 ya wapigakura watarajiwa milioni moja walisajiliwa; katika chaguzi za manispaa za mwaka 2004 idadi ilikuwa asilimia 77. 

Viwango vya chini vya usajili miongoni mwa vijana viliishia serikali katika kupendekeza usajili wa moja kwa moja na upigaji kura wa kujitolea. Vyama vya Concertación huunga mkono usajili wa moja kwa moja, lakini hakuna mwafaka kuhusiana na upigaji kura wa kujitolea. Wao huogopa kwamba ushiriki wa jumla utaanguka na kwamba gharama ya kifedha ya kampeni za kutafuta wapigakura itaongezeka, hivyo basi kutoa mazingira bora kwa vyama vya mrengo wa kulia. Upinzani, hasa UDI, hukataa usajili wa moja kwa moja na huunga mkono upigaji kura wa kujitolea.

Wafuasi wa mfumo uwili hudai kwamba umesaidia kuongozeka kwa sababu kuna miungano miwili mikubwa, mmoja katika serikali na mwingine katika upinzani. Hata hivyo, mtazamo huu hauna mwelekeo: Concertación kama muungano uliumbwa kabla ya mfumo uwili ulianzishwa, kama muungano ili kukabiliana na uongozi wa kiimla na kukuza demokrasia na wanasiasa ambao walikuwa wamejifunza kutokana na migongano yao ya awali (hali iliyoishia katika migongano na kuvunjika kwa demokrasia katika mwaka wa 1973) na walikubaliana kuhusu mbinu ya kuwashirikisha wasomi katika mfumo wa siasa ikilinganishwa na demokrasia ya miungano. Nchi hiyo inaoongozeka licha ya mfumo uwili, si kwa sababu yake.

Mfumo hauwezi kudumu kwa muda mfupi kwa sababu huharibu vyama vya kisiasa na kuzua miapaka kwa demokrasia, japo itakuwa vigumu kuufutilia mbali kwa sababu mabadiliko yanaweza kusababisha kukosekana kwa uhakika kuhusu athari ya ufuasi wa chama. Yatahitaji pia marekebisho ya kikatiba, kwa sababu sifa ya uwili ya Seneti imo katika katiba. Kuna mwafaka katika Kongresi kati ya Concertación na Muungano wa Chile kuhusu kuondoa maseneta ambao hawakuchaguliwa na marais wa awali kama wanachama wa kudumu.